Kwa mujibu wa Al-Jazeera, UNRWA imebainisha kuwa: karibu watu milioni moja wameyahama makazi yao huko Ukanda wa Gaza ndani ya muda wiki moja. Kwa upande mwingine, msemaji wa Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF amesisitizia ulazima wa kuwalinda watoto kwa mujibu wa sheria za kimataifa na kibinadamu na kutangaza kuwa: hali ya kibinadamu Gaza ni ya janga na maafa hasa kwa watoto na kwwamba zaidi ya watoto 700 wamepoteza maisha katika eneo hilo tangu yalipoanza mashambulizi ya Israel. Msemaji wa UNICEF ameendelea kueleza kuwa: hakuna mahali popote palipo salama kwa watoto katika Ukanda wa Gaza, na hakuna maji, chakula wala dawa.Wakati huohuo Shirika la Afya Duniani WHO limetahadharisha kuhusu kusambaratika kwa mfumo wa afya wa Gaza na kueleza kuwa: "hospitali za Gaza zimebakiwa na umeme wa saa chache tu na kulazimika kutumia majenereta ya umeme. Hali itakuwa mbaya zaidi akiba ya mafuta itakapokwisha, na matokeo yake yatakuwa mabaya zaidi na zaidi kwa wagonjwa, hasa kwa majeruhi wanaohitaji upasuaji na wagonjwa wa kitengo cha wagonjwa mahututi.
342/